Post AD

UEFA CHAMPIONS LEAGUE FINAL


*JUVENTUS vs REAL MADRID: NANI KUMFUNGA PAKA KENGELE?*




Leo ndiyo siku ya kumtafuta mbabe wa vilabu vyote vya Ulaya kwa mwaka 2016/17. Ni Fainali ya kipekee yenye msisimko wa kipekee.


Fainali hii imepikwa na kunakishiwa na rekodi tofauti tofauti huku Juventus akitazamwa kama timu yenye ukuta mgumu mno kuvunjwa kwa msimu huu wakati Real Mardrid wao wakisifika kupenya kwenye ukuta wowot na kuibuka na ushindi.

Katika mchezo wa leo Juventus anaingia uwanjani huku akipewa nafasi ndogo ya kuibuka na ushindi na wachambuzi wengi wa masuala ya soka wanaipigia chapuo Real Madrid ambayo imeimarika vilivyo katika michuano hii hasa kuanzia hatua ya mtoano.

Tumekuweka rekodi mbalimbal ambazo zimewekwa na vilabu hivi katika ngazi ya mashindano makubwa barani Ulaya.


Hii mara ya 19 kwa vilabu hivi kukutana katika michuano ya Ulaya na mech hii katika ya Juventus vs Real Madrid inakuwa ni mechi ya pili kuchezwa mara nyingi ikitanguliwa na ile ya Bayern  Munich vs Real Madrid ambao imechezwa mara 24

Katika mara 18 walizokutana Juventus vs Real Madrid, Wote wameshinda mara 8 kwa kila mmoja na sare ikiwa na mara mbili kwa kila mmoja.

Timu hizi zimkutana mara moja katika hatua ya fainali mwaka 1998 na Real Madrid aliibuka bingwa kwa ushindi wa goli 1 - 0 

Real Madrid ameshacheza mechi 14 za fainali ya michuano ya Ulaya na ameshinda mechi 11 kati ya hizo 14. Sasa anaenda kucheza fainali ya 15 dhidi ya Juventus.

Real Madrid anaingia fainali yake ya tatu katika misimu minne rekodi ambayo aliwahi kuiweka mwaka 1956 - 1960 ambapo aliingia fainali 5 mfululizo

Juventus ndiyo timu pekee ambayo haijafungwa hata mchezo mmoja katika ligi ya klabu bingwa barani Ulaya ikiwa imeshinda michezo 9 na kutoka sare michezo 3. Huku wakiruhusu magoli matatu tu katika michezo 12 ya klabu bingwa barani Ulaya


Juventus wameshinda fainali 2 tu (1985 na 1996) kati fainali 8 walizocheza, wakipoteza mfululizo fainali nne za mwisho 1997, 1998, 2003 na 2005


Toka amecheza mechi yake ya kwanza katika msimu wa 2007/08 Dani Alves amefunga magoli 10 na kusaidia magoli 25 ikiwa ni idadi kubwa kulikwa mabeki wote wa pembeni.


Cristiano Ronaldo amefungwa magoli 10 katika michuano hii kwa misimu sita mfululizo 


Zidane anaweza kubeba ubingwa wa Ulaya kwa mara ya pili akiwa kocha wa Real Madrid. Zidane pia alikuwa ni miongoni mwa wachezaji wa Juventus waliopoteza fainali ya 1998 dhidi ya Real Madrid.



Saa 21:45 wapenzi wote wa mpira wa miguu duniani wataelekea huko Cardiff katika dimba la Millenium Stadium. Je hisotria kumhukumu Jeventus au bahati itakuwa kwao? Muda ndiyo majibu kwetu. Usisahu kudondosha comment yako hapa chini.






Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni:

Chapisha Maoni